KWANINI WATU HULIA?

Jana
nilikuwa nasumbuliwa na swali hilo hapo. Nilikuwa nawaza mengi sana
kuhusu binadamu kulia. Nimejaribu kuatafuta vyanzo nakuta ni kama vile
MAKOSA, HUZUNI, FURAHA na mengineyo ambayo hayael;ezeki.
Ninajaribu
kufikiria sana suala hilo ingawaje naona kwa wtoto ni jambo ambalo
limekuwa katika eneo la makuzi yetu. Je nasi tunapolia tunatoa ishara
kwamba hatujakua kwahiyo tunahitajika kukua?
Nawaza
suala hili haya jawabu nakosa...na wakati mwingine nimewauliza wadogo
au watu wazima naona jawabu lao ni moja eti kawaida. Najiuliza
ingekuwaje pasingekuwepo na kulia? Nimeuliza hivi wewe Mume wako
amefariki, na unajua hataweza kurejea tena kwani unalia? Nini
kinachokuliaza hasa?
Wewew umemkosea mtu
jambo lolote, na unajaribu kumwomba msamaha, eti huku unalia na
kuangusha mchozi, kuna uhusiano gani kati ya kulia na makosa yako>?
Iwapoumemkosea rafikiyo, ndugu au wazazi kwanini unalia? Kuna siri gani
katika kulia kwetu wandamua
No comments:
Post a Comment