JINI MAHABA LINANISUMBUA....
Naomba niwekee hii habari Kwa wana mange's blog wenzangu wanisaidie. Nimekuwa nikisumbuliwa na jini mahaba Kwa mda mrefu sasa. Mwanzoni nilikua sijui Ila kwenye maisha yangu nimekua nikiota nafanya mapenzi na wanaume tofauti tofauti nikiwa ndotoni. Nikiwa na boyfriend tunapendana sana mwanzoni , tukikaa Kama mwezi hivi ananiacha au Mimi mwenyewe namchukia kupita kiasi namuacha.
Nikamweleza rafiki yangu mmoja yeye akanishauri anipeleke Kwa mganga, nilipofika huko ndio nikaambiwa Nina jini mahaba, niliogopa sana kwani ndio ilikua Mara yangu ya kwanza Kwa mganga, na pili kuambiwa Nina Jini.
Nina mengi sana Ila Kwa ufupi tangia siku hiyo Mimi nikawa Wa kuhangaika Kwa waganga tofauti tofauti, Mara Kwa Ustaadh wananisomea dua, mara kanisani bila mafanikio. Sasa nikienda Kwa mganga siku hiyo ndio balaa ananijia, Mara usiku naona jini linanishika Kwa nguvu linanifanya mapenzi, Mara linataka kunikaba, mara linaniambia tumezaa watoto siondoki nakupenda, Mara linanikandamiza kichwa etc, hapa Jana limetoka kunitisha limevaa kanzu nyeupe, yaani kila ukifika usiku nawaza sijui Leo atakuja, nasali tu nalala, Ila akinitokea ndio silali Tena Kwa uoga, Leo nimeamka saa Tisa usiku mpaka now asubuhi ndio nalala.
No comments:
Post a Comment